Baadhi ya Mashabiki wa Arsenal wameshauri kiungo Mesut Ozil auzwe baada ya mchezaji huyo kutoka Ujerumani kuripotiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watatu waliokataa kukatwa 12.5% katika mshahara wao ili kulinda uchumi wa klabu kutokana na janga la Virusi vya Corona, kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Mail.

Ozil analipwa mshahara mkubwa zaidi kuliko mchezaji yoyote ndani ya Arsenal akiwa anapokea Pauni 350.000 kwa juma lakini amekataa kukatwa 12.5% jambo ambalo baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wamelipokea tofauti sana, huku wengine wakishauri ni bora auzwe.

Wachezaji wengine waliokataa kukatwa 12.5% katika mshahara wao hawajatajwa ingawa suala hili sio la kimkataba, bali ni maamuzi ya mtu binafsi.

Kwa upande mwingine, Mesut Ozil amechangia Pauni 237,000 nchini Brazil kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji.

Mama Rwakatare kuzikwa na watu 10 kanisani kwake
Van Persie afichua kilichomuondoa Arsenal