![](https://dar24.com/wp-content/uploads/2020/04/ee6d0ab0c2e740edba246a82a58ad88c_18.jpg)
Serikali nchini Uganda imeanza kugawa msaada wa chakula jana kwa raia milioni 1.5 walio katika mazingira magumu zaidi wakati ambao shughuli zimesitishwa.
Waliopata chalula hicho cha bure ni wale walio athirika na hatua ya kusitishwa shughuli katika mji mkuu Kampala ili kudhibiti virusi vya corona.
Msafara wa malori sita yaliyokuwa na mifuko ya unga wa mahindi, maharage na chumvi ulianzishwa na mawaziri wa serikali na kuelekea kitongoji cha Bwaise.
Hadi kufika sasa, Idadi ya jumla ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona nchini Uganda ni 48 na hakuna kifo kilicho ripotiwa kutokana na ugonjwa huo.