Urusi pamoja na mataifa yanayozalisha mafuta kwa wingi duniani (OPEC) yamekubaliana kupunguza kiwango cha uzalishaji mafuta kwa takribani mapipa milioni 10 kwa siku ili kuidhibiti bei iliyoporomka kutokana na janga la kirusi cha corona.

Punguzo hilo, ambalo liliafikiwa kwenye mkutano wa jana wa mataifa hayo ni sawa na asilimia 10 ya kiwango cha kawaida  na makubaliano hayo yalifikiwa baada ya siku nne za mazungumzo.

Saudi Arabia inasema huenda punguzo hilo likakata uzalishaji wa mapipa milioni 12.5 kwa siku, kwa sababu ya kiwango kikubwa cha uzalishaji kutoka nchi hiyo, Kuwait na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Awali mazungumzo ya uzalishaji wa mafuta duniani yalikuwa yamekwama kutokana na mzozo na Mexico, lakini ufumbuzi ulipatikana baada ya mataifa wanachama wa OPEC kuliruhusu taifa hilo kupunguza mapipa 100,000 tu kwa mwezi.

TMA yatahadharisha mvua kubwa kwa mikoa 7
Wagonjwa wapya 14 wa Corona waongezeka Tanzania