Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Gervas Nyaisonga ambaye pia ni askofu Mkuu Jimbo Katoliki Mbeya amesema katika kupambana na maambukizi ya corona wamesitisha huduma za sakramenti, Ubatizo na ndoa
Kwa mujibu wa Rais huyo wa TEC shughuli zote zilizosimamishwa zitalejeshwa baada ya serikali kutangaza kumalizika kwa ugonjwa wa covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
Askofu Nyaisonga alitangangaza uamuzi huo jana mkoani Mbeya wakati akiendesha misa takatifu ya jumatatu ya Pasaka iliyofanyika katika kanisa la Parokia ya Roho Mtakatifu Ruanda.
”Nimeagiza Mapadri kusitisha shughuli zote za ndoa na ubatizo katika kipindi hiki ambacho kuna janga la Corona ,shughuli hizo na nyingine zitasitishwa mpaka hapo serikali itakapo tangaza kuwa janga hili la Corona limekwisha” amesema Askofu Nyaisonga
Aidha amewataka waumini wa kanisa hilo kuhakikisha wanafuata maelekezo ya serikali na wataalamu wa wizara ya afya yanayotolewa kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo.