Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul ameitaka Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuwatumia Maafisa Utamaduni wa ngazi za Mikoa, Wilaya na Halmashauri kutoa elimu ya masuala ya hakimiliki kwa wasanii na makundi mbalimbali.

Ametoa agizo hilo alipotembelea COSOTA  kufahamu majukumu  na mikakati yao katika kurahishisha utoaji wa huduma na ukusanyaji wa mirabaha ambapo aliwasihi kuongeza kasi katika kutoa elimu ili waweze  kukusanya vizuri.

‘’Jitahidini kuongeza kasi katika kutoa elimu kwa wadau kwa kuwatumia Maafisa Utamaduni kutoa elimu kwa wasanii na kwa nyie Maafisa wa COSOTA na gawaneni mikoa kila mmoja awe na jukumu la kuwasiliana na afisa utamaduni wa mkoa fulani kwa lengo la kusaidia kutoa elimu na kwa mambo ambayo hayajakamilika kama  marekebisho ya kanuni harakisheni kukamilisha,’’amesema Gekul.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania Andrew Shirima amesema majukumu mbalimbali ya COSOTA ni pamoja na kufafanua kuhusu mchakato wa upatikanaji wa mfumo wa ukusanyaji wa mirabaha  na namna mfumo huo utakavyo kuwa unafanya kazi na kurahisisha ukusanyaji wa mapato.

‘Mwezi huu wa Julai tumesaini mkataba na TTCL kwa ajili ya mfumo waliyouandaa wa kuuza kazi mbalimbali za Sanaa ikiwemo filamu ambapo utakuwa unauza filamu kwa viwango vya kimataifa kama ilivyo Netflix na jukumu la COSOTA katika mfumo huu ni kulinda hakimiliki kwa kazi zote zitakazowekwa katika mfumo huo,’’amesema Shirima.

Watu 5,429 watiwa mbaroni
Waziri Mkuu: Anayetaka achanje