Msanii kutoka katika lebo ya Live Fast, Live Good (LFLG) inayomilikiwa na Billnass, Country Boy amesema anatarajia kutoa albam yenye collabo nzito za kimataifa.

Rapa huyo ambaye wimbo wake ‘Turn Up’ bado ni gumzo, amesema albam yake inayosimamiwa utayarishaji wa mwisho na Harmy B itaingia mtaani mapema mwakani ikiwa na collabo kubwa ikimjumuisha pia Patoranking kutoka Nigeria.

“Albam yangu nzima mastering itasimamiwa na Harmy B. Ujue yule Hermy ni kama bro (kaka) anapenda muziki wangu lakini kuna makubaliano tumeyafanya ili kukamilisha, ujue ile ni kazi yake,” Country Boy amefunguka kupitia The Avanue ya TBC.

Aidha, mkali huyo ameongeza kuwa kuchelewa kutoka kwa albam hiyo ni kutokana na kutokamilika kwa collabo na wasanii wengine wa nje ya Tanzania.

“Albam nitatoa mwakani, ilikuwa tuachie mwaka huu lakini kwasababu ya ukubwa wa mastering kwa Harmy B na pia tunaitaji kupata collabo kubwa. Tayari tuna collabo iliyothibitishwa na Pantoranking tunasubiri atutumie vocal zake,” alisema.

Mkali huyo aliongeza kuwa wako kwenye mpango kuwashirikisha kwenye albam hiyo Khaligraph Jones na mbabe wa michano, melodi na mashairi Nyanshiski wote kutoka Kenya.

Uchanguzi Kenya bado kitendawili
Kenyatta amjibu Raila baada ya kujiondoa mbio za urais