Hatimaye msanii Harmonize amevunja ukumya kuhusu kuachana kwake na msanii Country wizzy aliyekuwa chini ya Label yake Konde Music Worldwide.

Harmonize ametolea ufafanuzi juu ya fununu zilizoenea kuwa nyota huyo alimnyang’anya gari Country Wizzy punde baada ya kumalizika kwa makubaliano yao ya kikazi.

“Kuhusu Country kuondoka na mimi kutomlipisha pesa, lengo halikuwa mimi kupata kitu, lengo lilikuwa ni sisi kutimiza ndoto zetu kama vijana, inawezekana lengo lilikuwa halijatimia lakini inapofikia muda na yeye anatamani kusaidia vijana wengine hilo ni jambo la kuungwa mkono,” amesema Harmonize.

“Kuhusu kurudisha gari tulikuwa na makubaliano ya pande zote mbili, kama ambavyo nimesema sisi sote ni vijana wenye malengo ya kufika mbali. Hata yeye alirudisha kwa kuelewa Konde Gang ni kampuni, kuna wadogo zake hapa ambao wanaweza kuwa na uhitaji zaidi yake yeye! Ndio maana baada tu ya kurudisha haikupita hata week akanunua gari yake mpya,” amesema Harmonize.

Harmonize ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na kipindi cha xxl katika shamra shamra za kuelekea kwenye kilele cha tamasha lake la Afro East Carnival linalotarajiwa kuanza kufanyika leo Machi 4 na kumalizika Machi 5, 2022.

Cedric Kaze: Tutacheza kwa tahadhari kubwa
Geita Gold wakanusha kuuza MECHI