Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Philipe Coutinho anatazamwa kama mchezaji wa kipekee ambaye atakuwa na nafasi kubwa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha FC Barcelona na kurejesha umuhimu wake msimu huu.
Kwa mujibu wa Gazeti la The Marca la Hispania, Coutinho sasa anatarajiwa kucheza mechi nyingi zaidi chini ya kocha Ronald Koeman, kikosi ambacho kwa siku za hivi karibuni kimeonekana kupungua ubora.
Coutinho amerejea akiwa fiti na tayari ameshaanza kucheza mechi na kikosi chake cha Barcelona akitokea benchi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambayo walipoteza, dhidi ya Bayern kwa mabao 3-0.
Coutinho anamaliza mkataba wake wa sasa na Barcelona mwaka 2023, na msimu ujao utakuwa muhimu zaidi katika maisha yake ya soka, ili kujua kesho yake.
Barcelona wanaweza kufanya maamuzi msimu ujao wa majira ya joto, ikiwa wasalie na nyota huyu au wamuweke sokoni.
Mshambuliaji huyo alitumia mwaka mmoja kwa mkopo kwa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, akifanikiwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kujikuta kwenye mkwamo wa majeraha na hakuwa kwenye kiwango kizuri.