Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko – CPB, imesema inaenda kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Mazao na Nafaka kwa ujumla kwa kutenga Sh. Billioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa mazao kutoka kwa Wakulima hapa nchini.

Aidha Bodi hiyo imetangaza fursa kwa wakulima wote nchini kulima mazao mengi msimu huu kwani Bodi hiyo inaenda kunu nua mazao hayo kwa wingi na kwa bei ya soko.

Akizungumza mara baada ya ziara ya bodi hiyo kutembelea miradi yao  iliyopo Kanda ya Ziwa Mwaza mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi aliyeongea kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo Kapenjama Ndile alisema wanaenda kufanya mapinduzi makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika Shirika hilo.

‘’Tunaenda kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Mazao na Nafaka kwa ujumla tunaenda kununua mazao ya zaidi ya Sh. Billioni 100 kutoka kwa Wakulima wa hapa nchini,’’ amesema Ndile.

Aidha Ndile aliwataka wakulima hapa nchini wazalishe mazao mengi kwani CPB itanunua mazao hayo kwa bei ya soko hivyo itatoa fursa kwa Watanzania kuuza mazao yao katika Bodi hiyo ili waweze kujikwamua Kiuchumi.

‘’CPB ni kimbilio kwa Wakulima tunanunua mazao kutoka kwao, lakini tunaongezea mazao thamani kwa kuchakata mazao kupitia viwanda vyetu vilivyopo katika baadhi ya Mikoa’’, amesema Mkurugenzi huyo wa Bodi hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema kipaumbele cha kwanza ni chakula na usalama wa Chakula, ndio maana Serikali iliunda Bodi ya Nfaka na Mazao Mchanganyiko ili kuwe na usalama wa chakula.

Aidha Ndile alisema Bodi hiyo inaendelea kujenga viwanda ikiwemo Kiwanda cha kuchakata Muhogo kitakachojengwa katika Jiji la Mwanza na Kingine kitajengwa Handeni Tanga.

Aidha Mkurugenzi huyo wa Bodi alisema kuwa wataendelea kupanua Viwanda vilivyopo na kuajili wataalamu wa viwandani lengo ni kupanua wigo wa uzalishaji ili waweze kuuza bidhaa ndan I ya nchi na nje ya nchi.

‘’Tuna viwanda Vingine vilivyomo Arusha ambapo kuna Kiwanda cha kuchakata Mahindi, Ngano, kiwanda kingine kipo Iringa kinachakata Mahindi na Dodoma kinachakata Mahindi Alizeti’, amesema Linde.

Naye Mjumbe wa Bodi hiyo Fadhili Ngajilo amesema kuwa kuwa Bodi hiyo imepania kuleta mabadiliko makubwa kwa Watanzania kwa kufungua milango ya biashara kupitia CPB.

Amesema kuwa hivi sasa Bodi hiyo imetengeneza utaratibu wa kuwatambua madalali wa mazao kama wafanyabiashara rasmi kwaajili ya kurahisisha biashara kati ya wakulima na Bodi hiyo.

‘’Bodi  hii imeingia kwenye ushindani wa biashara kwa kufanya biashara na mataifa ya nje  ila tutaboresha kwa viwango vya Kimataifa’’, amesema Ngajilo.

Amani ya Sudan: Hakuna dalili ya kusitisha mapigano
Ujenzi wodi wagonjwa mahututi nchini unaendelea