Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, amemtaka rais wa klabu hiyo Florentino Perez kumsajili Andre Silva wa FC Porto.
Ronaldo amemuomba Perez kufanya hivyo, kwa lengo la kupunguza gharama ambazo huenda zikatumika kwenye mpango wa usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu ya Juventus Paulo Dybala, itakapofika mwishoni mwa msimu huu.
Ronaldo anaamini mshambuliaji wa FC Porto Andre Silva ana vigezo vinavyotosha kuitumikia klabu ya Real Madrid, na ada yake ya usajili itakua nafuu zaidi ya Dybala ambaye anaamini itakua ni vigumu kumng’oa Juventus Stadium.
Paulo Dybala
Thamani ya usajili wa Dybala imetajwa na gazeti la El Mundo Deportivo la nchini Hispania kufikia Euro milioni 110, ambayo ni kubwa zaidi ya ile ya Silva ambaye atasajiliwa chini ya hapo.