Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC Cristiano Ronaldo, usiku wa kuamkia leo aliweka rekodi akiwa katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2020) kati ya Ureno dhidi ya Ukraine.

Katika mchezo huo kikosi cha Ureno kilishindwa kupaparika mbele ya wenyeji wao Ukraine, kwa kukubali kufungwa mabao mawili kwa moja.

Bao la kufutia machozi la Ureno lililofungwa na Ronaldo, ndilo lilimpa nafasi ya kuandika rekodi ya kufikisha mabao 700 katika michuano yote aliyocheza mpaka sasa.

Ronaldo amefikisha idadi hiyo ya mabao, baada ya kucheza michezo 976, katika ngazi ya vilabu pamoja na timu yake ya taifa.

Mwishoni mwa juma lililopita, nahodha huyo wa Ureno alifikisha mabao 699 katika mchezo dhidi ya Luxembourg, ambao Ureno ilishinda mabao matatu kwa sifuri.

Katika mchezo wa jana dhidi ya Ukraine, mshambuliaji huyo alifunga bao la kufutia machozi dakika ya 72 kwa penalti na kuufanya mchezo kumaizika kwa mabao mawili kwa moja, huku mabao ya Ukraine yakipachikwa wavuni na Roman Yaremchuk dakika ya sita na Andriy Yarmolenko dakika ya 26.

Image may contain: 2 people, text

Kwa rekodi hiyo, Ronaldo anaingia kwenye orodha ya wachezaji nguli waliofunga mabao 700 na zaidi kabla ya kustaafu, akiungana na akina  Josef Bica, Romario, Pele, Ferenc Puskas na Gerd Muller waliotamba kwa kufunga mabao enzi zao.

Nguli huyo amefunga mabao matano akiwa Sporting Lisbon, Man United (118), Real Madrid (450), Juventus (32) na 95 kwa Ureno.

Aliyechonga fimbo ya Nyerere achonga na ya Magufuli
Wakulima Rukwa waliozulumiwa, kulipwa fedha na Serikali