Cristiano Ronaldo ni kama amekula amini ya kubaki Real Madrid hadi atakapotundika viatu vyake vya soka miaka kumi ijayo.

Wakala wa mchezaji huyo ameiambia SkyNews kuwa taarifa zinazoendelea kuwa anatarajia kuihama timu hiyo mwishoni mwa msimu huu sio za kweli. Amesema mchezaji huyo hana tatizo lolote na Real Madrid na kwamba ana furaha ya kutosha akiwa katika klabu hiyo.

“Ni mchezaji bora zaidi wa wakati wote, na nina uhakika ataichezea Real Madrid kwa miaka mingine minne, mitano, sita, saba ijayo. Atamaliza soka lake huko, ana furaha akiwa Los Blancos. Atatundika viatu vyake vya soka akiwa na miaka 40,” alisema wakala huyo wa Ronaldo.

Ronaldo 2

 

Kulikuwa na taarifa kuwa Ronaldo ana mpango wa kurudi Manchester United au kujiunga na timu ya Paris Saint – Germain (PSG), taarifa ambazo zimekanushwa rasmi.

Don Jazzy atangaza Kuachana na Uimbaji Kuanzia mwaka 2016
Wanaume 1500 wajitangaza Kuwa Mashoga Mkoani Iringa, Wanafunzi waongoza