Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Mali, Bakary Sako amejiunga na klabu ya Crystal Palace ambayo ni moja ya vilabu 20 vitakavyoshiriki ligi kuu ya soka nchini England, msimu wa 2015-16 kuanzia mwishoni mwa juma hili.

Sako mwenye umri wa miaka 27, amejiunga na The Eagles baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Wolves ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza nchini humo.

Winga huyo alijiunga na Wolves mwaka 2012 akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya St Etienne na kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini England huku akicheza ligi daraja la kwanza, alifanikiwa kufunga mabao 36 katika michezo 118.

Sako anakua mchezaji wa tano kusajiliwa huko Selhurst Park baada ya kutanguliwa na Yohan Cabaye, Alex McCarthy, Patrick Bamford pamoja na Connor Wickham.

Spurs Wajitutumua Kwa Charlie Austin
Oliseh Amfungia Safari Mshambuliaji Wa Liverpool