Chama cha Wananchi (CUF) kimekanusha vikali taarifa zilizosambazwa na watu ambao hawajajulikana kwenye mitandao ya kijamii kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki.

Akiongea na ITV, Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mawasiliano na Umma wa chama hicho, Ismail Jusa amesema kuwa taarifa hizo zina lengo la kuvuruga amani na usalama wa nchi kwa kutengeneza taharuki.

Jusa ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuchukua hatua stahiki kwa waliopika na kusambaza habari hizo kwa kuwa mbali na kuwa kiongozi wa chama na mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif ni Kiongozi wa ngazi za juu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

“Yeyote aliyekuwa nyuma ya kusambaza uvumi huu hakuwa na nia njema. Na utaona kama ina malengo ya kisiasa kwa sababu taarifa yenyewe imehusishwa kwamba eti tukio hilo limetokea baada ya kujaribu kuwashawishi wajumbe wa vikao vyake vya CUF eti wasaini waraka wa kutaka uchaguzi urudiwe, jambo ambalo halipo,” alisema Jusa.

Taarifa hizo za kugushi zilizosambaa ziliwekewa nembo ya mtandao wa Facebook wa ITV, hali iliyokilazimu kituo cha ITV kukanusha vikali kuhusika na taarifa hiyo.

Maalim Seif azushiwa Kifo

Katika hatua nyingine, Jusa alieleza kuwa msimamo wa CUF kuhusu uchaguzi wa Zanzibar uko wazi kuwa hakuna kurudia uchaguzi na kwamba mshindi ambaye wanaamini ni Maalim Seif atangazwe.

Picha: Profesa Jay Aanza na ‘Kazi Tu’
Magufuli atinga Feri, awapa wavuvi namba yake ya simu, awaahidi mambo matatu