Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Prof. Ibrahim Lipumba, leo Desemba 4, 2017 kimeweka bayana kuhusiana na aliekuwa Mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia ambaye alichukua uamuzi wa kujivua uanachama na vyeo vyote ndani ya chama hicho na kujitangaza rasmi kuhamia CCM.

Ambapo Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma CUF, Abdul Kambaya amesema kuwa Mtulia amepaka doa chama chao na wananchi kwa ujumla huku kwani kuhama kwake chama kwa madai yakuwa nikutokana na kumuunga mkono Rais ni sababu zisizokuwa naa mashiko hata kidogo.

Mtulia amechukua uamuzi huo baada ya kufunguka ya moyoni na kukubaliana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli na kusema kuwa anaridhishwa na utendaji wake.

‘Sioni haja ya kuendelea kuwa mpinzani hivyo ni bora kumuunga mkono Rais’’ Amesema Mtulia

Aidha Mkurugenziwa Habari, Abdul Kambaya amelaumu maamuzi yaliyochukuliwa na Mtulia na kumuita msaliti kwani ameondoa uaminifu kwa wanachama  wa  jimbo lake la Kinondoni.
 

Ninje aisifu Kilimanjaro Stars, Mbarak kuikosa Zanzibar Heroes
Lissu amgusa Dkt Slaa, ‘Yuko Wapi?’