Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sayansi za afya (Cuhas), kimeanza kufanya utafiti kubaini chanzo cha wagonjwa wengi wa saratani na magonjwa yasioambukiza mikoa ya kanda ya ziwa.

Akizungumza kwenye mkutano na wandishi wa habari naibu Mkurugenzi wa utafiti Cuhas, Dkt Benson Kidenya amesema kwa sasa wana miradi 15 ya utafiti inayofanywa na chuo hicho.

“Tafiti zote zimeshaanza, saratani inashughulikiwa na taasisi ya saratani kwa kushirikiana na Hospitali ya Bugando, tunataka kwenda ndani zaidi kuangalia kama kuna viashiria kwenye damu au vinasaba ili kujua nini kinasababisha watu wanapata magonjwa haya,” amesema Dkt. Kidenya.

utafiti huo unaanza ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli aliolitoa Julai, 2019 wakati akizindua miradi ya afya kwenye Hospitali ya Kanda Bugando(BMC).

Inaelezwa kuwa zaidi asilimia 60 ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam wanatoka kanda ya ziwa .

Kocha wa Plateau Utd aihofia Simba SC
Manara awatuliza mashabiki Simba SC