Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwl. Deus Seif amewataka Walimu nchini kuendelea kuwa waadilifu ikiwemo kujiepusha na udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne iliyoanza leo Novemba 4, 2019.
Mwl. Seif ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari na kudai kuwa vitendo vya udanganyifu havina faida bali vinaongeza tatizo kwa Taifa hivyo waepuke jambo hilo kwa kusimamia maadili yao ya kazi kitaaluma.
“Niwaombe Waalimu wenzangu tudumishe uadilifu na tuache haki itendeke maana kosa dogo la Mwalimu linaweza likawagarimu wanafunzi wote tuwaache wafanye mitihani maana kazi ya ufundishaji tumeshaimaliza tuepuke udanganyifu,” amebainisha Mwl. Seif.
JPM ateua mrithi wa CAG, Uchaguzi wa serikali za mitaa ‘hatari tupu’
Amesema hadhi ya ualimu inatakiwa kulindwa kwa kuhakikisha Mitihani hiyo inafanyika bila udanganyifu na kwa kufanya hivyo watakuwa hawakiweki chama katika kashfa ya namna hiyo na kutoa salamu za kheri kwa wanafuzni wote nchini.
Jumla watahiniwa 485,866 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2019 ambapo kati ya hao waliopo shule ni 433,052 na wakujitegemea ni 52, 814.