DaBaby anakabiliwa na mashtaka ya kesi ya jinai kwa kuhusishwa na kesi ya kumpiga mwanamume anayedai kuteseka kwa kujaribu kuwazuia wasaidizi wa rapa huyo kupiga video ya muziki katika eneo lake kutokana na kuepuka maamukizi ya Corona.
Rapa huyo amefunguliwa mashtaka ya uhalifu na ofisi ya mwanasheria wa wilaya huko Los Angeles kufuatia tukio lililotokea mapema mwezi Desemba mwaka jana 2021 ambalo linadaiwa kumsababishia majeraha mabaya Gary Pagar ambaye ni mmiliki wa jumba hilo walilopanisha.
Pagar aliwasilisha kesi kwa vyombo vya usalama mapema Februari, akidai alishambuliwa kwa kutekeleza sheria za msingi za kukodisha nyumba yake ambayo rapa Dababy alikodishiwa kwa ajili ya mapumziko mafupi ya likizo.
DaBaby na timu yake walikodishiwa jumba hilo kubwa ambalo Pagar amasimama kama mmiliki na msimamzi huko L.A na Pagar anasema aliambiwa itakuwa mahali ambapo rapa huyo na marafiki zake watakuwepo kwa ajili ya likizo fupi, ambapo pamoja na makubaliano aliwaweka wazi kuwa sheria za nyumba hiyo ina ukomo wa idadi ya wageni wanaopaswa kuingia.
Na kwamba hawapaswi kuwepo katika eneo hilo zaidi ya watu 12, jambo ambalo rapa huyo na timu yake walikubalianalo katika makubaliano ya awali wakati wakukodisha.
Baada ya kipindi cha wiki mbili Pagar anasema alibaini kwamba kulikuwa na zaidi ya watu 12, jambo lililompelekea kuilalamikia timu ya DaBaby kwa kukiuka makubaliano yao ya awali.
Ilipofika Desemba 2, anasema alitembelea nyumba hiyo yeye mwenyewe na kugundua kwamba walikuwa wakirekodi video ya muziki na kikundi kizima cha filamu na idadi kubwa ya watu ambao anakadiria kuwa walifika zaidi ya 40, jambo lililomfanya ajaribu kuwazuia kuendelea na shughuli hiyo kwa kuwa tayari wamevunja utaratibu.
Na hapo ndipo anapodai kuwa alianza kushambuliwa na mmoja wa wafanyakazi wa rapa DaBaby, sehemu ambayo kwa bahati ilinaswa kwenye video,Pagar anadai kuwa baada ya muda mfupi DaBaby alimuamuru mfanya kazi wake huyo kuacha kumshambulia lakini aliendelea kumpiga ngumi usoni hadi kumsababishia jino lake kung’oka.
Inaonekana baada ya sakata hilo Pagar aliziendea mamlaka kuwasilisha malalamiko yake juu ya shambulio hilo, na sasa kesi hiyo inashughulikiwa kwa bidii ili kuhakikisha haki inapatikana.