Rapa DaBaby amekaa kwenye ‘headlines’ baada ya kuenea kwa taarifa za rapa huyo kuwa alishtakiwa kwa kosa la jinai baada ya Gary Pager, meneja wa mali, kumshutumu yeye na timu yake kwa kumshambulia na kumng’oa jino.
Shambulio hilo linalodaiwa lilitokea Los Angeles Desemba 2020 wakati wa kurekodi video ya muziki ambapo kulikuwa na tofauti ya idadi ya watu ambao walipaswa kuwepo katika eneo hilo.
Kufuatia kuenea kwa kasi kwa taarifa hizo hatimaye rapa DaBaby amejibu kwa mara ya kwanza kuhusu madai hayo.
Kupitia tweet na video alizochapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, DaBaby anasema Pager ni “Mtu mweupe mbabe.”
Katika video hiyo iliyoambatana na nukuu yake, ameonekana kukarisirishwa na kitendo cha kusambazwa kwa taarifa hizo ambazo amedai kuwa ni za uongo licha ya kufikishwa kwenye mamlaka za usalama nchini humo.
“Mtaendelea kuwaamini watu wa aina hii na kuwasaidia kuyaua mafaniko na uwepo wangu, na anaweza pia kupata sapoti ya kumsaidia kuiangamiza nafasi yangu.
Katika kipindi hiki ‘Wacha Tufanye DaBaby aonekane kama mtu mbaya,’ tunaye Gary Prager mbabe wa kizungu anayejivunia kuwadanganya TMZ na LAPD, bila kujua kuwa amenaswa na kamera.” amesema DaBaby.
Katika video iliyopatikana kupitia TMZ, inayoonesha sehemu ndogo ya ghasia hiyo, anaonekana zaidi rafiki wa DaBaby, Thankgod Acute, akimkandamiza Pagar na kumsukuma chini na si DABaby mwenyewe kama ripoti za awali zilivyoarifu.
Baada ya purukushani hizo DaBaby aliamuru Acute amuache mshtaki, hatimaye Pagar anasema alipata majeraha mabaya Kutokana na hali hiyo, jambo lililomfanya amfungulie Acute mashtaka ya wizi na uhalifu.
Kwa upande mwingine, katika taarifa zinazoendelea kuwa rapa DaBaby anahusishwa na kesi ya mauaji ya Jaylin Craig ya mwaka 2018 huko North Carolina zimeibua taswira mpya ambapo video za tukio ambazo hazijawahi kuonekana za mauaji hayo zimepatikana na Rolling stone.
Katika video hiyo rapa huyo anaonekana akifyatua risasi punde baada ya marumbano na anayedaiwa kuwa ni marehemu Jaylin.
Kuenea kwa video hiyo pengine pakazalisha mchakato mpya wa uchunguzi wa chanzo cha kifo cha Jaylin ili kubaini ukweli uliojificha ikiwa mhusika ni DaBaby au La.