Kituo cha afya cha Dabalo mkoani Dodoma kimepokea msaada wa vifaa tiba pamoja na majengo katika kuendelea kukabiliana na huduma za dharura za Afya ya mama na mtoto.
Msaada huo wenye gharama ya Shilingi milioni 615,205,539 umetolewa na shirika la Kimataifa la UNFPA kwa msaada wa Denmark kupitia mradi wa RMNCH wa Serikali ya Tanzania na umepokelewa na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Angelah Kairuki.