Mahakama ya Hakimu Mkazi Migori nchini Kenya, leo imemhukumu kifungo cha maisha jela mwanamke mwenye umri wa miaka 22, mfanyakazi wa ndani kwa kumbaka na kumpa ugonjwa wa zinaa mtoto wa kiume wa bosi wake.

Akisoma humu hiyo, Hakimu Mwandamizi, Raymond Langat ameeleza kuwa kulikuwa na vielelezo vya kutosha kuwa Machi 30, 2019 mwanamke huyo alitenda kosa hilo na kumuambukiza kwa makusudi mtoto huyo wa kiume.

Hakimu ameeleza kuwa Mahakama imefikia uamuzi wa kutoa adhabu hiyo baada ya kujiridhisha kuwa mshtakiwa alikuwa anatumia dawa za kutibu ugonjwa wa zinaa, hivyo alikuwa na nia ya kumuambukiza mtoto huyo.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mtoto huyo ambaye hivi sasa anapatiwa matibabu maalum, alipata madhara makubwa ya kisaikolojia kutokana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa Citizen TV, Mshtakiwa huyo amepewa siku 14 za kukata rufaa kama hajaridhishwa na uamuzi huo wa mahakama, vinginevyo atatakiwa kutumikia kifungo cha maisha jela.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 18, 2019
Rais wa zamani wa Misri afariki baada ya kuanguka mahakamani

Comments

comments