Kuwa ndugu wa mtu maarufu duniani kama muigizaji wa Kenya Lupita Nyong’o kunaweza kuwa chanzo cha umaarufu wako pia ambao utakuletea furaha ama kero unapokutana na jamii yenye mitazamo tofauti.

Dada wa Lupita Nyong’o, Zawadi ameumizwa na swali aliloulizwa na mhudumu wa hotel ya kifahari ‘Tribe Hotel’ nchini Kenya aliyemfananisha na ‘mama mzazi’ wa Lupita Nyong’o.
Zawadi

Zawadi hakupenda kabisa jinsi mfanyakazi huyo alivyomzeesha kutoka kuwa dada hadi kuhisi anaweza kumzaa Lupita Nyong’o.

“Nilimuuliza kama ninaonekana mzee kiasi hicho. Akasema, hapana..hapana ni kwa sababu mnafanana. Kwahiyo hiyo inanifanya niwe mama yake?” Aliuliza Zawadi.

Zawadi alienda mbali zaidi na kueleza jinsi anavyokwazwa na maswali ya watu mbalimbali anapokuwa katika sehemu za umma, wote wanamuuliza maswali ya kumhusisha na Lupita Nyong’o wakati yeye anataka siku moja achukuliwe kama Zawadi na sio ndugu yake Lupita.

“Not a single day goes by, no matter where I am (hospital, market, restaurant, street, gym, you name it) without being asked…Are Lupita’s sister?. I pray that one day I can just be seen as Zawadi, an individual. Not #NyongosDaughter or #LupitasSister. Sigh. I am tired,” alitweet.

Zawadi Nyong’o ni mwandishi na mjariamali mwenye ndoto ya kufanya makubwa kama dada yake ambaye yuko kwenye spotlight ya dunia, Hollywood.

Inspector Haroun Ajibu Tuhuma Za Kumdhurumu Luten Karama Na Kumbania
Navio Atangaza Ujio Mpya Wa Kundi Lake Na Album