Dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ambaye anafahamika kwa jina la Kim Yo-Jong atahudhuria ufunguzi wa mashindano ya Olympics 2018 yanayofanyika Korea Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Serikali ya Korea Kusini, Kim Yo-Jong ataambatana na viongozi wa ngazi za juu wa Korea Kaskazini.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa viongozi wa ngazi za juu wa Korea Kaskazini kuzuru Korea Kusini tangu vita kati yao ya mwaka 1953.
Kim Yo-Jong anatajwa kuwa mmoja kati ya washauri wanaosikilizwa zaidi na Kim Jong Un katika hatua za maamuzi na ni mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha propaganda.
- Kiongozi wa Boko Haram atoa video baada ya jeshi la Nigeria kutoa tamko
- Maofisa 2 watiwa mbaroni kwa kula rushwa
Hatua hii inaonesha mwanga zaidi wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya nchi hizo wakati ambapo bado kuna taharuki ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya nyuklia.