Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kuomba michezo mitatu ya kirafiki sawa na dakika 270 wakati timu hiyo itakapoweka kambi ya maandalizi ya msimu wa 2023/24 nchini Uturuki.

Michezo hiyo mitatu itawahusisha wachezaji wote wakiwemo wa zamani na wapya ambao wamesajiliwa kwa ajili ya msimu ujao 2023/24.

Robertinho amesema michezo hiyo mitatu inamtosha kutengeneza kikosi imara kitakachokuwa tishio Afrika msimu ujao.

Robertinho amesema tayari amewashawasilisha ripoti ya msimu ujao kwa uongozi, ambayo atatumia wiki tatu katika Pre Seasson kuisuka timu.

Ameongeza kuwa, amewataka viongozi kuanza utaratibu wa kutafuta timu hizo za kucheza nazo huko Uturuki kwa ajili ya kuangalia ubora wa kila mchezaji.

“Pre Seasson yangu itakwenda sambamba na kucheza michezo ya kirafiki tukiwa Uturuki ambako tunatarajiwa kuweka kambi fupi ya maandalizi ya msimu ujao.

“Hivyo tukiwa huko tutacheza michezo mitatu ya kirafiki, maalum kwa ajili ya kutengeneza timu itakayocheza kwa muunganiko mzuri.

“Ninatarajia kuona mabadiliko ya kikosi cha kwanza kwa kuingiza maingizo mapya ya wachezaji, hivyo ni baada ya kufanya usajili,” amesema Robertinho.

Dkt. Kikwete atembelea Kliniki ya Biashara Sabasaba
Sheikh Jassim akaribia kuimiliki Man Utd