Matajiri wa jijini Dar es salaam, Klabu ya Azam FC inayonolewa na Kocha Kali Ongala ina dakika 270 za kazi ndani ya Uwanja kwenye michezo ya ushindani katika Michezo mitatu itakayocheza ndani ya mwezi huu April.
Kwenye kete hizo tatu mbili watakuwa nyumbani pale Uwanja wa Azam Complex na mchezo mmoja watakuwa ugenini.
Ngoma inaanza kupigwa leo Jumatatu (April 3), itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Azam Complex huu ni mchezo wa hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.
Atakayepoteza mchezo huo ana muda wa kulipa kisasi kwenye mchezo wa Ligi ambapo Azam FC itamenyana tena na Mtibwa Sugar April 7, huu utakuwa ni mchezo wa mzunguko wa pili utachezwa uwanjani hapo.
Ruvu Shooting dhidi ya Azam FC unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro Aprili 22, utakamilisha mwendo wa dakika 270 za kazi ndani ya April.