Tunisia na Senegal zina nafasi nzuri ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia 2018, endapo zitashinda michezo ya mwishoni mwa juma hili, huku Ivory Coast na Morocco zikikabana koo katika safari ya Urusi.

Tayari Misri na Nigeria zimeshafuzu kucheza fainali hizo, ambazo zinasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani kote.

Senegal watapambana na Afrika kusini katika mchezo wa kundi D, na watalazimika kupambana ili kufikia lengo la ushindi dhidi ya Afrika kusini ambao watakua nyumbani siku ya ijumaa.

Mchezo huo ambao utachezwa katika mji wa Polokwane utakua wa marudio, baada ya shirikisho la soka duniani FIFA kubaini mchezo wa kwanza kutawaliwa na vitendo vya upendeleo ambavyo vilionyeshwa na mwamuzi kutoka Ghana Joseph Lamptey ambaye amefungiwa.

Mchezo huo wa awali Afrika Kusini waliifunga Senegal mabao mawili kwa moja.

Senegal na Afrika kusini zitarudiana katika mchezo utakaochezwa mjini Dakar kati kati ya juma lijalo.

Kocha mkuu wa Afrika kusini Stuart Baxter amesema anaamini kikosi chake kinadharauriwa kuelekea katika mchezo dhidi ya Senegal, lakini suala hilo halimpi shaka na badala yake anaendelea kuwaandaa wachezaji wake.

Kwa upande wa mchezo wa Ivory Coast dhidi ya Morocco, kocha kutoka nchini Ufaransa Herve Renard atakua na kazi kubwa ya kupambana na taifa lililomuajiri kabla ya kutimkoa mjini Rabat, kwa kuhakikisha anawapa ushindi Simba wa Milima ya Atlas.

“Ninaamini mchezo utakua mgumu, lakini sina budi kuwahimiza wachezaji wangu ili wakamilishe ushindi ambao utatuvusha na kutupeleka kwenye fainali za kombe la dunia 2018,” Amesema Renard.

Kwa upande wa kocha kutoka nchini Ubelgiji Mark Wilmots ambaye bado anahaha kukaa sawa kwa kuweka heshima ya kuwa kocha wa Ivory Coast kufuatia kufungwa na Gabon katika mchezo uliopita, atakua na kazi ya ziada ya kuhakikisha anashinda dhidi ya Morocco.

Michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia ukanda wa Afrika itakayochezwa kesho ijumaa.

Kundi B Algeria v Nigeria

Kundi D – South Africa Vs Senegal

 

Jumamosi.

Kundi A – Tunisia v Libya

Kundi A – DR Congo v Guinea

Kundi B – Zambia v Cameroon

Kundi C – Gabon v Mali

Kundi C – Ivory Coast v Morocco

Kundi – Congo v Uganda

 

Jumapili.

Kundi E – Congo v Uganda

Kundi E – Ghana v Egypt

 

Jumanne.

Kundi D – Senegal v South Africa

Kundi D – Burkina Faso v Cape Verde

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 10, 2017
Seif Rashid Abdallah (Karihe) aongezwa Zanzibar Heroes