Daktari aliyetoa tahadhari ya kwanza ya mlipuko wa Virusi vya Corona, nchini China, Li Wenliang (34) amefariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi hivyo.
Wenliang ambaye alikuwa Daktari katika Hospitali moja Wuhan alianza kutoa tahadhari ya mlipuko wa Virusi vya Corona kwa madaktari wenzake tangu Desemba mwaka jana, lakini alionywa na mamlaka kwa kusambaza habari za uongo.
Alipojaribu kuwatahadharisha madaktari wenzake kujikinga na maambukizi hayo, aliitwa na Idara ya Usalama na kutuhumiwa kuchapisha taarifa za uongo zilizokuwa zinasababisha usumbufu.
Hadi sasa Virusi vya Corona vimeua takriban watu 600 nchini China.