Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Heamedia Medical Clinic Dkt. Hery Mwandolela amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kila mmoja kuhakikisha anapima afya yake mara kwa mara huku akitaja sababu zinazosababisha ugonjwa wa moyo.
Amesema kuwa ni vyema kila mtu akafahamu namba saba muhimu kwa afya yake na kusisitiza kitendo cha kuchelewa kutambua ugonjwa mapema kunasababisha gharama kubwa zaidi.
Dkt. Hery Mwandolela amesema hayo kwenye mahojiano maalum wakati anazungumza kwenye maonyesho ya Sabasaba ya Biashara ya kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa lengo la uwepo wake kwenye banda hilo kwanza unalenga kuwakumbusha wananchi mbalimbali kutambua umuhimu wa kupima afya mara kwa mara kwani inasaidia kupunguza gharama za matibabu.
Aidha, Dkt. Mwandolela amesema kuwa pamoja na kutoa huduma kwa kiwango cha hali ya juu wameweka gharama nafuu ambazo kila mmoja anaweza kumudu ukilinganisha na maeneo mengine.
Hata hivyo, ameongeza kuwa magonjwa kama ya kupanda kwa shinikizo la damu na kisukari huweza kuja bila dalili yeyote na wakati mwingine yanagundulika baada ya mhusika kupata madhara makubwa.
“Njia pekee ya kukabiliana na magonjwa haya ni kujenga tabia ya kupima afya zetu hata kama hatusikii dalili zozote za ugonjwa, kwani hii itsaidia kugundua tatizo mapema na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana nalo.
-
Video: Zitto, Polepole watunishiana misuli mtandaoni, ‘Mzee wa kurukia treni kwa mbele ushaanza
-
Video: Madude kumi yaliyomng’oa Mwigulu, Utabiri wa Lema watimia, Nape, Zitto wamkaribisha uraiani
-
Mengi atoboa siri ya kutunga kitabu chake