Daktari wa klabu ya Young Africans, Sheikh Mngazija ameweka wazi kuhusu hali ya kiungo mshambuliaji kutoka nchini Angola Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo ‘Carlinhos’ ambaye kwa kipindi kirefu hajaonekana dimbani.

Daktari Mngazija amesema kiungo huyo aliyesajiliwa mwezi Agosti 2020 na kisha kulakiwa kwa shangwe na wanachama na mashabiki wa Young Africans wakati akiwasili nchini, alikuwa na matatizo mawili.

Amesema ‘Carlinhos’alikua anasumbuliwa na nyama za nyuma ya paja na uvimbe ulioota kwa mbele ya paja la kulia, maradhi ambayo yalishindwa kumpa nafasi ya kujumuika na wenzake kwa majuma kadhaa yaliyopita.

Hata hivyo Mngazija amesema tayari kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, ameshaanza mazoezi mepesi na huenda akawa sehemu ya kikosi pindi ligi itakaporejea.

“Carlinhos alikuwa akiumwa vitu viwili kwa wakati mmoja hizo nyama za nyuma ya paja na uvimbe ulioota kwa mbele ya paja hilo la kulia, lakini ameanza mazoezi mepesi.” Amesema Daktari Mngazija.

Katika hatua nyingine Dakrati Mngazija ameeleza maendelea ya mshambuliaji kutoka nchini Burkina Faso Yacouba Sogne aliyeumia nyama za paja katika mchezo wa nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Amesema mshambulaiji huyo bado anaendelea kupatiwa matibanbu na wanatarajia kurudisha hospitali kwa ajili ya kumfanyia vipimo.

“Tunatarajiwa kumpleka tena hospitali ili kumfanyia vipimo vingine zaidi kufahamu shida ambayo inamsumbua ni ipi, na kwa nini ameshindwa kupona katika matibabu ya awali na baada ya hapo ndio ataanza tiba mpya na kufahamu atakuwa nje kwa muda gani.” Amesema Daktari Mngazija.

Mfahamu Sebastien Desabre anaewanyima usingizi Simba SC
Matola: Morrison haumwi ‘MSHIPA WA NGIRI’