Mshambuliaji kutoka nchini Argentina, Angel Di Maria jana jioni alifanyiwa vipimo vya afya huko mjini Doha nchini Qatar ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha uhamisho wake kutoka Man Utd kuelekea kwa mabingwa wa soka wa Ufaransa Paris St Germain.

Tukio la kupimwa afya kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, lilifanywa kwa siri kubwa na maafisa wa klabu ya PSG, lakini mmoja wa madaktari wa kituo cha afya alichokwenda Di Maria alishindwa kujizuia na kuanika hadharani taarifa hizo.

Daktari huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, alianika taarifa hizo katika mtandao wa kijamii wa Twitter dakika chache baada ya Di Maria kuonekana akiongozana na viongozi wa klabu ya PSG katika kituo cha afya cha Aspetar.

“#AngelDiMaria yupo Aspetar, Doha kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya yake, kwa lengo la kukamilisha usajili wake wa kuihama @ManUtd na kwenda @PSG.” Daktari huyo alitweet.

Taarifa hizo iliambatana na picha za Di Maria ambaye alionekana akiwa na kijana wa kiarabu aliyekuwa amevalia vazi la kanzu na kilemba kichwani kwake.

Man Utd wamedhamiria kumuuza Di Maria katika kipindi hiki huku wakijipanga kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Hispania na klabu ya Barcelona, Pedro.

Nightclub Aliyokuwamo Drake Yashambuliwa Kwa Risasi, Wawili Wauwa
Ni Ubabe-Ubabe CCM na Ukawa, Nani Zaidi?