Daktari wa Chelsea,  Eva Carneiro amewashukuru mashabiki waliomtia moyo baada ya kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho kuishambulia timu ya matabibu akisema kwamba ni ‘wajinga’.
Katika sare ya 2-2 dhidi ya Swansea katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya England, Mourinho alichukizwa na kitendo cha Carneiro kuingia uwanjani kumtibu Eden Hazard na kutumia muda mrefu ilihali dakika zikisalia chache.
Wakati huo Chelsea walilazimika kubaki 9 uwanjani na Swansea wakapata fursa ya kulisakama lango la Chelsea.
Mourinho alisema daktari huyo hakuelewa mchezo.
Carneiro amesema: “Napenda kuwashukuru watu wote walionipa moyo. Kiukweli nimepata faraja sana”.

Messi, Suarez Kuisaidia Barcelona Leo?
Neymar Nje Siku 14