8 years agoComments Off on Dani Alves: Kwaheri Juventus FC
Beki wa pembeni kutoka nchini Brazil Dani Alves, amethibitisha rasmi kuachana na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC, baada ya kuwatumikia kwa msimu mmoja.
Alves alikua hajasema lolote kuhusu kuondoka kwake mjini Turine, licha ya uongozi wa Juventus kutoa taarifa za kusitisha mkataba na mchezaji huyo waliemsajili akitokea FC Barcelona mwanzoni mwa msimu wa 2016/17.
Alves mwenye umri wa miaka 34, alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Juventus, lakini mwishoni mwa msimu uliopita alianzisha mazungumzo ya kutaka mkataba huo uvunjwe ili atimize melengo aliyojiwekea.
Lengo kubwa linalotajwa kuwa sababu ya kumuhamisha Alves klabuni hapo, ni kutaka kujiunga tena na aliyekua meneja wake alipokua FC Barcelona Pep Guardiola, ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Man City ya England.
“Ninapenda kuwashukuru watu wote waliofanikisha maisha yangu nikiwa Juventus FC kwa kipindi cha mwaka mmoja, ninawashukuru wachezaji wenzangu tuliocheza kwa ushirikiano mkubwa, tumefanikiwa kwa pamoja mpaka kucheza fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya…,” Alves ameandika katika akaunti yake ya Instagram.
“Leo uhusiano wetu wa karibu unakwisha rasmi, na nitakuwa katika majukumu mengine kisoka, daima nitaendelea kukumbuka mchango wangu nilioutoa nikiwa na Juve, ambayo ni moja ya klabu kubwa nilioitumikia kwa dhati ya moyo wangu.”