Mwenyekiti wa Tottenham Hotspur, Daniel Levy amesema ilifanya makosa kupitisha maamuzi ya kuwaajiri Jose Mourinho na Antonio Conte kama makocha klabuni hapo, kwani klabu hiyo ilihitaji kurejea mizizi yake na kocha mpya, Ange Postecoglou.

Mwezi Machi mwaka huu, kocha wa zamani wa Juventus, Conte alikua kocha wa pili mwenye medali kadhaa za washindi kuondoka Kaskazini mwa London katika muda wa zaidi ya miaka mitatu.

Pia walimfukuza Mourinho miaka miwili iliyopita baada ya Mreno huyo kuletwa kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino.

Levy amekuwa akizongwa sana siku za nyuma, huku baadhi ya mashabiki wa Spurs wakimlaumu kutoshinda medali yoyote tangu mwaka 2008.

“Nataka kushinda kama kila mtu mwingine,” alisema Levy kwenye kongamanola mashabiki.

“Kuchanganyikiwa kwa kutoshinda na shinikizo kutoka kwa baadhi na wachezaji na sehemu kubwa ya msingi ya mashabiki ambayo tunahitaji kushinda, tunahitaji kutumia fedha, tunahitaji kuwa na kocha mkubwa, jina kubwa. Na iliniathiri.”

Pochettino alitimuliwa mwaka 2019, miezi mitano tu baada ya kuiongoza Spurs kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kocha huyo alikuwa na kibarua cha kuinoa Paris Saint Germain kabla ya kuinoa Chelsea msimu huu wa joto.

“Nilikuwa nimepitia kipindi ambacho tungekaribia kushinda, na Mauricio tulipitia wakati nzuri sana,” aliongeza Levy.

Mkutano Polisi wa kike Duniani IAWP wafungwa rasmi
Hatma ya AFCON 2027 Jumatano