Mshambuliaji Danny Ings alikua miongoni mwa wachezaji waliowahi kusajiliwa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili majira ya kiangazi kwa England, jana jioni.
Ings alifanikiwa kuihama klabu ya Liverpool na kujiunga na Southampton kwa mkopo na huenda akasajiliwa jumla mwishoni mwa msimu wa 2018/19, endapo ataonyesha kiwango kitakachoridhisha akiwa St Mary’s.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports cha England, mshambuliaji huyo amejiungana The Saint kwa gharama ya Pauni milioni 20.
Southampton wametoa kiasi cha Pauni milion 18, na Pauni milioni 2 zitalipwa mwishoni mwa msimu, endapo kiwango cha mshambuliaji huyo kitaridhisha, ili kukamilisha usajili wa jumla.
Ings anaondoka Liverpool baada ya kuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kwanza msimu uliopita, kufuatia kusajiliwa kwa mshambuliaji kutoka nchini Misri Mohamed Salah.
Meneja wa Southampton Mark Hughes anaamini mshambuliaji huyo bado ana uwezo mkubwa wa kucheza soka na kufunga mabao, na ana uhakika wa jambo hilo kudhihirishwa kwa vitendo katika msimu huu.
Hughes amesema Ings ana uhakika wa kuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha cha kwanza cha Southampton, na huenda akaanza kumtumia katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa ligi utakao wakutanisha dhidi ya Burnley mwishoni mwa juma hili.
Akiwa na klabu ya Burnley katika msimu wa 2014/15, Ings alionyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao na kuwa kivutio katika soko la usajili wa mwishoni mwa msimu huo, Liverpool walifanikiwa kuipata saini yake, kwa kuamini huenda angewafaa, lakini ilikua tofauti na matarajio yao.
Mpaka anaondoka Anfield kwa mkopo, Ings alikua ameshacheza michezo 14 na kufunga mabao 3.