Beki wa kati wa Young Africans Andrew Vicent ‘Dante’ amesema atatumia michezo iliyosaliwa na Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe La Shirikisho (ASFC)  kumshawishi kocha Luc Eymael, kumjumuisha kwenye kikosi chake cha kwanza.

Tangu arejeshwe kikosini baadhi ya changamoto yake ya madai kumalizwa na GSM, Dante amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi mbele ya Lamine Moro, Kelvin Yondani, Ally Mtoni na Said Juma Makapu

Hata hivyo beki huyo aliyetua Young Africans Mtibwa Sugar mwaka 2015, amesema anaamini ligi itakaporejea, atakuwa na nafasi ya kurejea kikosini.

“Unajua muda kama huu kila mtu hafanyi mazoezi ya timu, tukienda tunaenda kuanza wote kwa pamoja ndio maana nakuambia tunaenda kuanza upya”

“Nitatumia nafasi hii vizuri kurejea katika kikosi cha kwanza, naamini kiwango changu kwamba suala la kucheza ni la muda na ndio maana siku zote siachi kufanya mazoezi, nitafanya mazoezi mchangani na nitacheza mpira,” alisema

Pamoja na kutoonekana uwanjani kwa muda mrefu, mashabiki wengi wa Young Africans bado wameonyesha kuwa na imani na beki huyo kisiki ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanaosubiri mikataba mipya. Mkataba wa beki huyo unamalizika mwishoni mwa msimu.

Mwamnyeto kubaki Coastal Union
Joto la Uchaguzi Mkuu: Madiwani 8 wa CUF watimkia CCM