Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Dar es Salaam yatakosa umeme kwa saa nane leo Oktoba 24, 2022 kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Taarifa iliyotolewa leo na Shirikia hilo imetaja sababu ya kukosekana nishati hiyo ni kutokana na matengenezo yanayotarajiwa kufanyika ya mtambo namba mbili wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Songas uliopata hitilalfu.

Aidha Taarifa hiyo imesema baadhi ya maeneno ambayo yataathiriwa kwa kukosa umeme wataje wa maeneo yote watatumiwa ujumbe mfupi(sms) kwenye simu zao.

Shirika la umeme Tanzania linahakikisha linaendelea kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma ya umeme ni ya uhakika na wa kutosha kwa muda wote.

Ally Kamwe: Tunashukuru kupata sare
Ahmed Ally: Siamini kama wamechomoka