Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa tahadhari ya kuwa na upungufu wa  huduma ya maji kwa wakazi wa Bagamoyo na Dar es Salaam kuanzia leo Jumatatu machi 9,2020.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo inasema upungufu huo unatokana na mareboresho wa matambo wa maji wa Ruvu chini.

Taarifa hiyo imeainisha maeneo yatakato athiriwa na upungufu huo wa maji ni pamoja na Baganoyo ,Tegeta, Bunju, Mbezi chini Afrikana, Tank Bovu, Mbweni, Kawe, Goba, Makongo na Lugola.

Aidha maeneo mengine amabyo yataathirika na maboresho hayo ni Magomeni, mikocheni, Masaki, Sinza, Kijitonyama,Mwananyamala, Kinondoni,Kariakaoo, Upanga na Kisutu,

”Sababu ya upungufu ni maboresho ya miundombinu katika katika mtambo wa uzalishaji maji wa ruvu chini” imesema taarifa hiyo.

Wanawake Mexico kuadhimisha siku ya 'bila wanawake' kwa kutotoka nje
Waziri mkuu Sudan anusurika kuuawa