Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza uamuzi wa Serikali wa kutenga jumla ya hosptali 25 katika mkoa huo ambazo zitatumika kama hatua ya awali kukabiliana na ugonjwa wa COVID 19.

Amesema mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa huo atatakiwa kufika kwenye moja ya hospitali hizo ili kuweza kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali.

Amesema Hospitali zilizotengwa zipo za binafsi na zile za Serikali zikiwemo hospitali zote za rufaa.

Akitaja Hospitali hizo Amesema Ilala kuna jumla ya hospitali nane (8) ambazo ni, Amana, Buguruni, Mnazi Mmoja, Muhimbili, Hindu Mandal, Agha khan na Regency.

Huku Kinondoni kukiwepo na Hospitali sita (6) ambazo ni Mwananyamala, Magomeni, Kliniki ya IST, TMJ pamoja na Rabininsia.

Temeke kukiwa na Hospitali nne (4), Temeke, Mbagala Rangi Tatu, na Yombo TOHS huku Ubungo nako Hospitali nne zilizotengwa ambazo ni Sinza, Kimara, Mloganzila, BOCHI.

Na Kigamboni Hospitali tatu ambazo ni Vijibweni, Kigamboni, na Agha Khan.

Makonda amesema Katika hospitali hizo wataalamu watatoa huduma ya vipimo vya magonjwa mbalimbali yote na wakibaini hakuna ugonjwa ndipo watawasiliana na maabara ya kitaifa ili kuweza kuchukua sampuli na kupima ili kubaini kama ameathirika na Corona.

Amesema lengo ni kusaidia wananchi wote waweze kupata vipimo vya ugonjwa huo hatari wa COVID 19.

Aidha, ameishukuru wizara ya afya pamoja na Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) mawili kwa kila wilaya na magari ya kusaidia timu za kupambana na Corona kila wilaya lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba hakuna mwananchi anayepoteza maisha kwa kukosa huduma.

Sakata la Clatous Chama latua TFF
Young Africans waanika usajili 2020/21