Jumla ya tuzo saba za umahiri katika uandishi wa habari nchini Tanzania – EJAT, zimeenda kwa waandishi nyota wa Dar24 Media katika usiku wa tuzo zilizotolewa Julai 22, 2023 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam.

Dar24 Media iliwakilishwa na Festo Lumwe aliyetwaa tuzo mbili, Stanslaus Lambat, Dauka Somba, Heldina Mwingira, Zuhura Makuka, Abel Kilumbu na Issa Ramadhani aliyeshika nafasi ya pili kwenye kipengere cha kundi la wazi.

Abel Kilumbu wa Dar24 Media katika tabasamu la tuzo

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya tuzo hizo kubwa zaidi za uandishi wa habari nchini Tanzania, kushuhudia chombo cha Habari za mtandao kikitawala tuzo hizo kwa waandishi wake saba kushinda kwenye vipengele mbalimbali.

Mgeni rasmi kwenye sherehe za 14 tuzo za EJAT ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ikulu, Balozi Ombeni Sefue ambaye amewataka Wanahabari nchini kuhakikisha wanapata maarifa ya kutosha kuhusu masuala mbalimbali kabla ya kuhabarisha au kuelimisha umma.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio wakati wa utoaji wa tuzo hizo.

Zuhura Makuka wa Dar24 Media akipokea idadi za tuzo.
Stanslaus Lambat wa Dar24 Media akifurahia tuzo.
Heldina Mwingira wa Dara24 Media katika uso wafuraha ya tuzo.
Dauka Somba wa Dar24 Media akiwa na furaha wakati akipokea chake (Tuzo).
Festo Lumwe wa Dar24 Media aliyeibuka na tuzo mbili.
Hongera Dar24 Media Team – Taarifa bila mipaka.

Utoaji wa Habari uzingatie vyanzo vya kuaminika - Nape
Arsenal warudisha majeshi Aston Villa