Dar24 Media, kupitia kampuni  yake mama ya DataVision international leo Desemba 22, 2017 imezindua rasmi kampeni  endelevu ijulikanayo kama ‘’Tuko Pamoja’’  inayolenga kusaidia jamii hasa vijana wadogo wenye  umri chini ya miaka 18, na leo wamekuja na kampeni  yao inayoitwa Okoa Maisha ya Mariam.

Uzinduzi wa kampeni ya Tuko Pamoja, Okoa Maisha ya Mariam imelenga kuarifu Umma wakiwemo wadau kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusu msichana mdogo Mariam (16) anayesumbuliwa na ugonjwa kidaktari ujulikanao kama ”Intestinal Obstruction”  na kuwaomba watanzania kwa ujumla kuhusika katika kampeni hiyo kwa kuchangia kwa namna moja au nyingine ili pamoja  kuokoa maisha ya Mariam.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Masoko wa DataVision International,  ambaye pia ni Msemaji wa Dar24, Teddy Ntemi Qirtu katika ukumbi wa Serena ambako uzinduzi huo ulifanyika rasmi.

Aidha amewaomba wananchi na wadau kwa ujumla kumchangia mtoto Mariam ili aweze kwenda nchini India kufanyiwa matibabu, mara baada ya jitihada za madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Muhimbili kushindwa kutatua tatizo hilo na kupelekea kumfanyia oparesheni kumi bila mafanikio.

Ambapo ameeleza kuwa  gharama za kuratibu shughuli nzima ya matibabu hayo akiwa nchini India ni kiasi cha shilingi milioni 44 za kitanzania.

Hivyo amewaomba wananchi kuungana na Dar24 kupigania maisha ya  Mariam kwa kuchangia fedha kupitia M-lipa, tigo pesa, Airtell Money na Mpesa kwa kuandika namba ya kampuni 400700 na kumbukumbu namba 400700 au kupitia akaunti ya benki ya CRDB kwa akaunti namba 0150021209500 jina la akaunti ni Data Vision International – Tuko Pamoja.

Hata hivyo wamechukua nafasi hiyo kuwashukuru wadhamini wao, Serena Hotels, ID Card Solutions, Kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola, Kampuni ya MacLeans BeneCIBO, M-
Lipa, Kampuni ya PR ya AMIFAN na OnDemand.

Ambao mpaka sasa wameonesha ushirikiano wa dhati kwa kushirikiana na uongozi wa Dar24 katika kufanikisha kampeni yao ya Tuko Pamoja okoa maisha ya Mariam.

Pia amewashukuru wale ambao tayari wamekwisha wasilisha michango yao kupitia mfumo maalumu wa Mlipa kama ambavyo imeelekezwa na kuwaomba wadau kuendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuokoa maisha ya Mariam.

Meck Sadick aingizwa kamati kuu Yanga
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 22, 2017