Katibu Mteule wa Serikali ya Wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Hussein Amri Aman, ameomba umma kukanusha taarifa zinazodai kuwa marehemu Maria Godian Soko aliyefariki katika ajali ya gari na kukimbizwa hospitalini alikuwa mjamzito.

Amir ameeleza kwamba marehemu Soko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya pumu na ndiyo sababu kuu iliyomfanya awe akimbizwe hospitali kwa gari ya msaada wa haraka”ambulance”.

“Marehemu Maria alikuwa na matatizo ya pumu ambayo yalimsababishia kifua kubana hadi kuzimia hivyo majira ya saa mbili kasoro tulifanya utaratibu wa kuita ambulance ya chuo na kumchukua hapa mabibo hostel kumpeleka hospitali ya chuo kwa matibabu zaidi”.

“Wakati taratibu za kumpeleka hospitali ya chuo zinaendelea ndipo ajali mbaya ikatokea pale riverside, taarifa zinazoendelea kusambaa kwamba marehemu alikuwa mjamzito anaenda kujifungua sio za kweli”. amesema Amir.

Katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Riverside imesababisha vifo vya watu watatu wakiwemo wanafunzi wawili, Maria Godian Soko (Mwaka wa kwanza COSS) na Steven E Sango  (CPE CoET mwaka wa pili) pamoja na dereva James.

Aidha katika ajali hiyo mwanafunzi mmoja wa mwaka wa tatu Abishai Nkiko (Bsc Industrial Engineering mwaka wa 3 CoET) hali yake ni mbaya na anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili.

 

 

Gerard Deulofeu asajiliwa jumla Vicarage Road
Justin Kluivert kukamilisha usajili AS Roma