Rais Magufuli, amemtengua Katibu Tawala wa Kisarawe, Mtela Mwampamba na kumteua Mwanana Msumi, aliyekuwa Afisa Tawala wa Wilaya kuchukua nafasi hiyo.
Rais Magufuli amesema kuwa Katibu Tawala huyo amekuwa akikiuka maadili ya utumishi wa Umma, ikiwemo kuchukua wake za watu.
“Huyu DAS kuanzia muda huu aondoke Kisarawe akafanye kazi kwingine.Amekuwa akikiuka maadili ya utumishi wa umma na alishaonywa huko nyuma lakini ameendelea.Tena ninazo taarifa anachukua na wake za watu hapa kwa watani zangu,” amesema Rais Magufuli.
Baada ya kutengua uteuzi wa Mwampamba, Rais Magufuli aliuliza wakiwemo viongozi wa Mkoa wa Pwani wanaoongozwa na Mkuu wa mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo kuwa nani anafaa kuwa Katibu Tawala wa Kisarawe.
Ambapo Mkuu wa Mkoa alisimama na kutaja jina la Mwanana MSumi Baada ya kutaja jina hilo Rais Magufuli aliuliza kiwango cha elimu cha Sumi na kujibiwa ana Masters.Hivyo akamtangaza hapo hapo kuwa Katibu Tawala mpya wa Wilaya ya Sarawe.