Watu watatu wamepoteza maisha akiwemo Katibu Tawala (DAS) wa Wilaya ya Handeni, Comred Boniface Maiga Jumaa baada ya gari mbili kugongana Mkoani Dodoma.

Ajali hiyo ambayo ametokea leo Julai 11, majira ya saa saba usiku maeneo ya Vikonji Jijini Dodoma imesababisha majeruhi kadhaa akiwemo Mbunge wa Handeni, Omary Abdallah Kigoda.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ikihususha, gari la Omari Kigoda ambaye ni Mbunge wa Handeni na Bus aina ya Tata.

Gari la Kigoda lilikua na watu wanne akiwemo yeye mwenyewe, DAS, Dereva na Msaidizi wa Kigoda.Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea.

Imeelezwa kuwa Hali za majeruhi zinaendelea vizuri katika Hosptali ya Rufaa ya Dodoma. Mwili wa Marehemu Bonface Maiga upo Hosptali ya General.

Simba Queens yaisasambua Yanga Princess
Wasira: Hata Malaika angegombea na Bulaya 2015 angeshindwa, nagombea tena