Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), DataVision International imejipanga kupambana na changamoto ya mazingira kwa kuunga mkono kikamilifu kampeni ya uhifadhi wa mazingira, ambapo imepanda miti katika Shule ya Msingi ya Mikocheni iliyopo jijini Dar es salaam.

Kampuni hiyo imepanda miti katika Shule ya Msingi Mikocheni, karibu na Ofisi Kuu za DataVision International kwa lengo endelevu la kutoa elimu kwa uhifadhi wa mazingira ya shule hiyo.

Akizungumza mara baada ya kupanda miti, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Masoko wa DataVision International, Teddy Qirtu amesema kuwa kuhifadhi mazingira na Maliasili ni muhimu kwani Tanzania ni nchi inayoendelea katika ulimwengu wa kisasa,

Amesema kuwa DataVision International kwa kutambua jitihada za Serikali katika kuhakikisha nchi ina mazingira safi na salama kwa kizazi cha sasa na kijacho, hivyo imeamua kuunga mkono jitihada hizo kwa vitendo.

“Kama Kampuni ya TEHAMA inayojali zaidi kuhusu dunia ambayo teknolojia imeifanya kuwa kijiji, tunatambua kuwa uharibifu wa mazingira ni moja kati ya tatizo kubwa linaloikabili dunia hii ya kisasa ambalo linahitaji utatuzi wa haraka na madhubuti. ndiyo sababu tunaunga mkono kwa vitendo kampeni ya uhifadhi wa mazingira,” amesema Qirtu

Aidha, ameongeza kuwa Kampuni hiyo inaunga mkono kampeni ya serikali inayoendelea ya uhifadhi bora wa mazingira, ikiwa hivi karibuni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alitoa wito kwa sekta binafsi na watu binafsi kujiunga na jitihada za uhifadhi bora wa mazingira kwa kupanda na kutunza miti.

Hata hivyo, kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mikocheni, Salehe Makwiro ameipongeza kampuni ya DataVision International sio tu kwa kupanda miti hiyo bali pia kuwa sehemu ya mchakato wa kuitunza kwa mwaka mzima.

 

Video: Itazame ngoma mpya ya Dully Sykes 'Zoom'
Barcelona yalipa fadhila kwa Eric Abidal