Uongozi wa Klabu ya Manchester United unakaribia kufikia makubaliano na Mlinda Lango David de Gea juu ya mkataba mpya, kwa mujibu wa ESPN.
Mlinda Lango huyo anakaribia mwisho wa mkataba wake wa sasa na anaweza kuondoka Old Trafford bure mwishoni mwa msimu.
United, hata hivyo, wanaamini wako karibu na makubaliano ambayo yatamfanya De Gea kuongeza muda wake wa kukaa huku akipunguza mshahara wake wa kimsingi lakini kwa motisha kubwa inayohusiana na kiwango cha uchezaji.
Masharti mengi yamekamilika ingawa mazungumzo yanaendelea kuhusu jinsi mkataba huo ulivyopangwa.
United pia wana chaguo la kuweka nyongeza ya mwaka mmoja kwenye mkataba wake unaomalizika Mei, lakini kuna imani katika klabu masharti mapya yatakuwepo kabla ya hilo kuhitajika.
De Gea amekuwa namba moja muhimu kwa kocha, Erik ten Hag tangu kuwasili kwa Mholanzi huyo majira ya joto yaliyopita, na kucheza mechi 47 katika mashindano yote.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 amecheza mechi zaidi ya 500 tangu alipowasili kutoka Atletico Madrid mwaka 2011.