Bondia David Haye huenda akatangaza kustaafu mchezo wa ndondi kwa mara ya pili, baada ya kupoteza pambano lake la mwishoni mwa juma, kwa kuchapwa na Tony Bellew.

Haye alipoteza pambano hilo kwa KO, hali ambayo imeonyesha kuwasikitisha mashabiki wake ambao waliamini huenda angefanikiwa kushinda kirahisi.

Uchunguzi wa awali umebaini Haye alishindwa kuendelea na pambano hilo baada ya kuangushwa baada ya kuichapo kikali, kufuatia maumivu makali ya kisigino yaliyomuandama.

Baada ya mchezo huo bondia huyo kutoka nchini England alikimbizwa hospitali na ameshauriwa kufanyiwa upasuaji, hali ambayo inamuingiza katika hatari ya kutangaza kustaafu bila kupenda.

Katika mchezo huo Haye alipatwa na maumivu wa kisigino katika raundi ya sita, lakini alijitahidi hadi katika raundi ya 11 ambapo alikubali kichapo kitakatifu na kupelekea kocha wake kurusha taulo ulingoni kwa kuashiria amekubaliana na matokeo.

Kwa sasa bondia huyo yupo hospitali akiendelea kupatiwa matibabu na wakati wowote hii leo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.

Wakati huo huo promota Eddie Hearn amemshauri Haye kustaafu mchezo wa masumbwi ili kulinda heshima yake, pamoja na hali yake ya kiafya ambayo haitomruhusu kurejea ulingoni kwa kupambana kama ilivyokua siku za nyuma.

Kwa mara ya kwanza Haye alitangaza kustaafu ndondi Oktoba 11 mwaka 2011, baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Wladimir Klitschko, lakini aliamua kurejea na kuzichapa dhidi ya Mark de Mori Novemba 24 mwaka 2015.

Antonio Conte Awapa Somo The Blues
Video: Makonda asema vita ya dawa za kulevya haijawahi kumuacha mtu salama