Mchezaji Daud Milandu wa Geita Gold FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa Singida Big Stars kwa ajili ya kuinasa saini yake.

Mbali na Singida Big Stars, Wagosi wa Kaya, Coastal Union nao wanamfuatilia kwa karibu nyota huyo Milandu ambaye aliwahi kukipiga Ndanda, Fountain Gate, African Sports na sasa yupo zake Geita Gold.

Rafiki wa Karibu na mchezaji huyo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa katika Vyombo vya Habari amesema kuna timu ambazo zinamfuatilia kiungo huyo kwa ajili ya kupata saini yake.

“Kuna timu zaidi ya mbili zinamfuatilia Milandu miongoni mwa hizo ni Singida Big Stars, Coastal Union hivyo lolote linaweza kutokea na hata Geita Gold nao bado wanahitaji huduma yake,” amesema rafiki huyo

Kwa upande wa Afisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza kuhusu suala hilo alijibu kiufupi: “Kwa sasa dirisha la usajili bado hivyo subiri mpaka wakati ukifika.”

Mandonga kuzichapa na Mmalawi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 2, 2023