Aliyewahi kuwa meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes amesema anaweza akarejea Old Trafford iwapo atapewa nafasi hiyo, licha ya kufutwa kazi 2014.

Akizungumza katika kipindi cha Clare Balding cha BBC, Moyes amesema angefanya mambo tofauti iwapo angejua atahudumu kwa miezi 10 na sio miaka sita kama ilivyokuwa mkataba wake.

“Nilikuwa na wachezaji wazuri, walikuwa wameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya chini ya uongozi wa Sir Alex Fergurson katika msimu uliopita,” amesema.

“Ingechukua muda kubadilisha mfumo wa mchezo na hata wachezaji wangehitajika kubadilishwa na haya yote nisingengeyafanya kwa miezi kumi.”

Moyes alifutwa kama meneja United Aprili 2014 baada ya kuwaongoza kwa miezi 10 pekee.

Kabla ya hapo, alikuwa amekaa miaka 11 klabu ya Everton.

Maalim Seif Awatoa wasiwasi wazanzibari
IAAF Yamfungia Maisha Papa Massata Diack