Hatimae meneja wa klabu ya Sunderland David Moyes, ameshtuka na kuamini beki kutoka nchini Ufaransa Lamine Kone atamfaa katika mipango yake kwa msimu huu, baada ya uongozi wa Everton kutuma ofa ya kutaka kumsajili.

Moyes alikua amemuweka pembeni beki huyo ambaye alisajiliwa mwezi Januari klabuni hapo akitokea Lorient, jambo ambalo lilizua utata na kufikia hatua kwa Kone kuzungumza wazi katika vyombo vya habari kuhusu mustakabali wake kuwa shakani.

Moyes ameonyesha kwa vitendo kumuhitaji beki huyo mwenye umri wa miaka 27, kwa kukubali kumuongezea mshahara wa paund 50,000 kwa juma.

Everton walituma ofa ya Pauni milioni 14, ambayo waliamini ingetosha kumng’oa Kone ambaye alionyesha kutokua na furaha baada ya kuajiriwa kwa Moyes kama mbadala wa Big Sam aliyekabidhiwa kikosi cha timu ya taifa ya England mwezi uliopita.

Victor Valdes: Nilipokua Man Utd, Nilitamani Kustaafu Soka
Pau López Sabata Kuuwahi Mchezo Wa Kesho?