Nguli wa muziki kutoka Nigeria, Davido Adeleke maarufu kama Davido hatimaye ameachana na ukapera mara baada ya kuamua kumvisha pete ya uchumba mpenzi weke Chioma.

Tukio hilo limefanyika siku ya Ijumaa ya Septemba 13 na kuhudhuriwa na  watu wake wa karibu.

Katika hafla hiyo Davido ameweka wazi kuwa licha ya kumvalisha pete, Chioma amembebea ujauzito wake jambo ambali lilimfurahisha zaidi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Davido ameonesha tukio hilo zima.

Hata hivyo ujauzito huo utampatia Davido mtoto watatu, ambapo watoto wake hao wawili aliwapata kwa wanawake wawili tofauti ambao ni Aurora Imade Adeleke na Hailey Veronica Adeleke.

Davido na Chioma ni wapenzi waliodumu kwa muda mrefu na inasemekana kuwa wawili hao wanatarajia kufunga ndoa mapema mwakani nchini Nigera.

Tayari familia ya Davido na Chioma zimekutanishwa pamoja kwa ajili ya utambulisho ili waweze kufahamiana zaidi.

Mwenyekiti klabu ya Simba, Swedi Mkwabi ajiuzulu
Marais 10 Afrika washiriki mazishi ya Mugabe